DKT. NCHEMBA APOKEA RIPOTI ZA SENSA
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akipokea Ripoti za Sensa za Mgawanyo wa Idadi ya Watu kwa maeneo ya kiutawala na Idadi ya Watu kwa umri na jinsia kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba (katikati), baada ya kukabidhiwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali. Dkt. Albina Chuwa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma.