DKT. NCHEMBA APIGIA CHAPUO UWEKEZAJI MITAJI KUTOKA NJE NA LUGHA YA KISWAHILI NCHINI NIGERIA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiwa na Ujumbe wa Tanzania katika Ubalozi wa Tanzania, uliopo Abuja nchini Nigeria, ambapo yeye na ujumbe wake, akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango-Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi, wanashiriki Mikutano ya Nchi za Afrika (African Caucus Meetings), ukiwashirikisha Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Mhe. Dkt. Nchemba na ujumbe wake walipowasili katika Ubalozi huo, walilakiwa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Bi. Judica Nagunwa akiambatana na Mwambata Jeshi wa Ubalozi Brigedia Jenerali Julius Kadawi na Maafisa wengine waandamizi