DKT. NCHEMBA AKUTANA NA WATAALAMU WA TATHMINI YA UCHUMI KUTOKA SADC
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii licha ya kutokana na sera zake nzuri za kifedha na kiuchumi licha ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Dunia zikiwemo athari za Uviko 19 na mizozo ya kivita inayoendelea maeneo mbalimbali Duniani.
Amesema hayo jijini Dar es Salaam, alipokutana na kufanya mazungumzo na timu ya watalaam wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ofisi za Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.