DKT. NCHEMBA AIKARIBISHA TAASISI YA UINGEREZA KUWEKEZA NCHINI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameikaribisha Taasisi ya kifedha ya Uingereza inayojihusisha na uwekezaji (British International Investment) kufanya uwekezaji nchini katika sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo ya Nishati. Dkt. Nchemba, ametoa wito huo alipokutana na kufanya majadiliano na ujumbe wa British International Investment, katika Ofisi ya Hazina, jijini Dar es Salaam ambapo wameangazia mambo mbalimbali ya ushirikiano wa maendeleo.