DKT. NCHEMBA AIAHIDI JUMUIYA YA KIMATAIFA KUWA SERIKALI ITAONGEZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA KILIMO

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa kwamba Serikali ya Tanzania itaendelea kuwekeza fedha za kutosha kwenye sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao na kuifanya nchi kuwa ghala la chakula duniani. Mhe. Dkt. Nchemba amesema hayo wakati aliposhiriki, mdahalo wa viongozi wa ngazi ya juu wa nchi za Afrika, kuhusu chakula na kilimo, ulioandaliwa na Taasisi inayojihusisha na uhamasishaji wa masuala ya kilimo Barani Afrika (AGRA), kando ya mikutano ya Kipupwe iliyoandaliwa na Banki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ,jijini Washington D.C, Marekani.