DKT NATU: TANZANIA NA UNICEF KUENDELEZA USHIRIKIANO
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Watoto (UNICEF) anayehusika na Programu, Bi. Patricia Safi Lombo, ambapo wamejadili kuhusu namna ya kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali na Shirikika hilo hususan maendeleo ya huduma za jamii.
Dkt. Mwamba alisisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kushirikiana na UNICEF katika kutekeleza miradi inayolenga kuinua ustawi wa jamii na kukuza maendeleo ya kiuchumi nchini.
