DKT. NATU MWAMBA ATETA NA TIMU YA BENKI YA DUNIA

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Timu ya Benki ya Dunia Tanzania, ikiongozwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Bw. Nathan Belete, kuhusu Ushirikiano wa Maendeleo kati ya Tanzania na Benki hiyo hususan Utekelezaji wa miradi inayotekelezwa nchini, pamoja na miradi inayotarajiwa kufadhiliwa na Benki hiyo kupitia mzunguko wa IDA 21, tukio lililofanyika kando ya Mikutano ya Kipupwe ya IMF na Benki ya Dunia, inayofanyika Jijini Washington D.C, nchini Marekani.