DKT. NATU MWAMBA ASHIRIKI HAFLA YA WANAWAKE VIONGOZI ILIOANDALIWA NA BENKI YA DUNIA JIJINI WASHINGTON D.C
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, ameshiriki katika hafla ya kifungua kinywa iliyowakutanisha wanawake viongozi kutoka sekta mbalimbali, iliyoandaliwa na Benki ya Dunia kupitia Wakurugenzi Watendaji wake, Bi. Anna Bjerde na Bi. Anshula Kant, katika Ofisi za Benki hiyo jijini Washington D.C nchini Marekani, kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF inayoendelea jijini humo.
Tukio hilo limeendelea kukua kila mwaka na kuwa jukwaa muhimu la kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika uongozi na maendeleo ya kiuchumi duniani.
