DKT. NATU MWAMBA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MIKUTANO YA MWAKA YA BENKI YA DUNIA NA IMF WASHINGTON D.C-MAREKANI

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameongoza ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mikutano ya Mwaka (Annual Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF), inayofanyika Jijini Washington D.C nchini Marekani, yenye kaulimbiu ya “Foundations for Growth and Jobs”. Akiwa katika Ubalozi wa Tanzania nchini humo, Dkt. Mwamba alipokea Taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ubalozi kutoka kwa Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza, ambapo amempongeza Balozi na timu yake kwa kazi kubwa ya kuiwakilisha nchi na kuahidi kuwa Wizara yake itaendelea kuunga mkono juhudi zake za kusimamia biashara na ukuzaji wa uchumi wa nchi kupitia ushirikiano kati ya Marekani na Tanzania.