DKT. NATU MWAMBA AIPA CHANGAMOTO JUMUIYA YA KIMATAIFA KUSAIDIA NCHI ZA AFRIKA KUTEKELEZA SDGs
Bara la Afrika limeitaka Jumuiya ya Kimataifa kuweka nguvu ya pamoja kulisaidia Bara hilo kukabiliana na changamoto mbalimbali zitokanazo na athari za uviko 19, mabadiliko ya tabianchi pamoja na mizozo ya kivita inayotishia ustawi wa nchi mbalimbali kiuchumi na kijamii; na kukwamisha kasi ya utekelezaji wa ajenda ya Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030.
Wito huo umetolewa Jijini New York nchini Marekani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakati akihutubia wajumbe wa Jukwaa la Juu la Siasa la Umoja wa Mataifa kwa niaba ya Umoja wa Afrika, ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Umoja huo kwa mwaka 2023.