DKT. MWIGULU NCHEMBA AITA WAWEKEZAJI SEKTA YA UMEME NCHINI TANZANIA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewahimiza wawekezaji kutoka kila pembe ya dunia, kuwekeza katika sekta ya nishati ya umeme nchini Tanzania, ili kuzalisha nishati ya kutosha na ya uhakika ambayo itauzwa katika nchi mbalimbali ikiwa ni njia ya kukabiliana na changamoto ya uhaba wa nishati hiyo katika Bara la Afrika. Dkt. Nchemba ametoa wito huo Jijini Washington D.C, nchini Marekani, wakati akizungumza kwenye mkutano wa Mawaziri wa Fedha kutoka nchi za ukanda wa Kusini mwa Afrika, waliojadili kuhusu usalama wa nishati na namna ya kuishirikisha sekta binafsi kuwekeza kwenye uzalishaji wa nishati ya umeme na kutumia pia changamoto hiyo kama fursa ya kufanya biashara ya kuuziana nishati hiyo,