DKT. MWAMBA AKUTANA NA BALOZI WA UBELIGIJI NCHINI TANZANIA
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert, ambapo wamezungumza kuhusu kuendeleza ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na nchi hiyo.
Mkutano huo uliofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ulihudhuriwa pia na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Melckzedeck Mbise, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ubeligiji, Bw. Koenraad Goekint na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Ubeligiji, Bi. Fanny Heylen pamoja na wajumbe wengine kutoka Wizara ya Fedha na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.