DKT. MWAMBA AHAMASISHA WANAWAKE KUWA MABALOZI WA MABADILIKO

Wanawake wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi kushiriki na kupiga kura katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kifanyika mwezi Oktoba mwaka huu ili kutimiza haki yao ya kidemokrasia. Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Fedha, Bi. Fauzia Nombo, wakati akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, katika hafla ya kikundi cha wanawake wa Wizara cha Golden Women, iliyofanyika katika Ukumbi wa Mabele jijini Dodoma.