DKT. MPANGO AZINDUA MCHAKATO WA MAANDALIZI YA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa maagizo sita ya kuzingatiwa katika Maandalizi ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, ikiwemo kuimarisha uwezo wa uchumi uliopo na kulinda mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Alitoa maagizo hayo jijini Dodoma wakati wa akizundua Mchakato wa Maandalizi ya dira mpya ya Maendeleo ya Taifa 2050.