DKT. MPANGO AMUAGIZA WAZIRI WA FEDHA KUPITIA KODI YA MAJIKO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amemuagiza Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kuangalia uwezekano wa kupitia viwango vya kodi kwa majiko yanayotumia nishati safi ya kupikia hasa kipindi hiki ambacho maandalizi ya bajeti ijayo yanafanyika. Maagizo hayo ameyatoa wakati akifungua Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia, lililofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.