CAG KICHERE: BAJETI YA SERIKALI TOLEO LA MWANANCHI LAONGEZA UWAZI

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere, ameipongeza Wizara ya Fedha kwa kuandaa yaliyomo kwenye Bajeti ya Serikali kwa lugha nyepesi (Toleo la Mwananchi) kwa kuwa inamsaidia mwananchi kuielewa bajeti ya nchi. Bw. Kichere ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.