BWAWA LA MTERA LAFIKIRIWA KUTATUA KERO YA MAJI DODOMA

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akiaangalia kina cha maji ya Bwawa la Mtera lililopo Mpwapwa Dodoma, wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, ilipotembelea Bwawa hilo ili kuona uwezekano wa kuzalisha zaidi ya lita milioni 133 kwa siku kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa maji katika jiji la Dodoma.