Bi. OMOLO AWAPONGEZA TRAT KWA KUPUNGUZA MIGOGORO YA KODI NCHINI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akizungumza wakati wa Kikao chake na Watumishi wa Baraza la Rufani za Kodi (TRAT), katika ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam, ambapo amewapongeza kwa kazi nzuri ya kusimamia na Kusikiliza rufaa zinazotokana na uamuzi wa Bodi ya Rufani za Kodi (TRAB), Kutoa ushauri kwa wananchi waliopo kwenye migogoro ya kodi juu ya taratibu za kukata rufaa kupitia Baraza pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu Sheria ya Rufani za Kodi na sheria nyingine zinazohusiana na kodi.