BI. NOMBO: NJOONI MPATE ELIMU KWENYE BANDA LA WIZARA

Wizara ya Fedha imewataka wananchi wa mkoa wa Dodoma kutembelea Banda la Wizara hiyo ili kupata elimu ya fedha, pensheni na majukumu mbalimbali yanayofanywa na Wizara hiyo. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Usimamizi Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha Bi. Fauzia Nombo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Natu El-maamry Mwamba, kwenye maonesho ya kuelekea kilele cha maadhimiho ya siku ya wanawake duniani yanayofanyika katika viwanja vya Mashujaa, Jijini Dodoma.