BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA KUTOA SH. BIL. 398.7 KUJENGA SGR NCHI ZA TANZANIA -BURUNDI - DRC CONGO NA KUKUZA MTAJI WA BENKI YA KILIMO TANZANIA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Patricia Laverley, wakisaini hati za Mikataba miwili yenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 158.1 (sawa na shilingi za Tanzania, bilioni 398.7) kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Kimataifa wa Reli ya Kisasa (SGR) utakaoziunganisha nchi ya Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), pamoja na kuiongezea mtaji Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB), hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Bw. Emmanuely Lyimo na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.