BENKI YA DUNIA YAJITOSA KUSAIDIA UJENZI WA RELI YA KISASA NA KUKARABATI RELI YA KATI

Benki ya Dunia imeahidi kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi unaoendelea wa Reli ya Kisasa-SGR na ukarabati wa Reli ya Kati-MGR, kutokana na umuhimu wa miradi hiyo katika maendeleo na uchumi wa nchi. Ahadi hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete, aliyeongoza ujumbe wa Benki hiyo, walipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa na Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa.