BENKI YA DUNIA KUENDELEA KUSAIDIA MAENDELEO YA SEKTA BINAFSI TANZANIA
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru Taasisi ya Benki ya Dunia inayotoa mikopo na misaada kwa sekta binafsi (Internationa Finance Corporation-IFC), kwa kuwekeza zaidi ya dola za Marekani milioni 370 kwa ajili ya kuendeleza sekta hiyo nchini.
Dkt. Nchemba amesema hayo alipoongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano na Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Bw. Sergio Pimenta, kando ya mikutano ya Kipupewe iliyoandaliwa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la KImataifa (IMF), Jijini Washington D.C, nchini Marekani.