BALOZI WA DENMARK AMALIZA MUDA WAKE AMUAGA DKT. NCHEMBA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameishauri Denmark kuongeza masuala ya ushirikiano katika sekta za nishati, maendeleo ya sekta ya fedha na kukuza uwekezaji katika mpango wao mpya wa ushirikiano wa kimataifa unaoandaliwa na nchi hiyo. Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo wakati akimuaga Balozi wa Denmark nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Mette Dissing-Spandet, katika Ofisi za Hazina Ndogo, Jijini Dar es Salaam.