BALOZI OMAR ATOA WITO WA KUREJESHA MAADILI MEMA KATIKA JAMII

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ametoa wito kwa Watanzania kushirikiana katika kurejesha na kuimarisha maadili mema katika jamii, akisisitiza kuwa jukumu la kujenga jamii yenye maadili si la Serikali pekee, bali linawahusu wazazi, walezi, walimu, viongozi wa dini na kila mwanajamii. Mhe. Omar ameyasema hayo wakati wa hafla ya ugawaji wa zawadi kwa washiriki na washindi wa mashindano ya Sira ya Mtume Muhammad (SAW) yaliyoandaliwa kupitia Kampeni ya Rudisha Maadili kwa Jamii na Uzinduzi wa Huduma ya Daktari wangu kupitia Mfuko wa Bima ya Mufti, iliyofanyika katika Msikiti wa BAKWATA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.