BALOZI KHAMIS: SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR INAJALI WANANCHI

Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, itaendelea kuboresha huduma za jamii ikiwemo sekta ya afya kwa wananchi wake. Mhe. Balozi Omar ametoa kauli hiyo wakati akizindua Kituo cha Afya cha Kisasa cha Kinduni, kilicho gharimu shilingi bilioni 3.77, kilichokojengwa katika Wilaya ya Kaskazini B mkoa wa Kaskazini Unguja, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.