AICAD YATAKIWA KUENDELEA KUTUMIA TAFITI KUTATUA CHANGAMOTO ZA MAENDELEO.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, ameitaka Taasisi ya African Institute for Capacity Development (AICAD) kuendelea kuimarisha matumizi ya tafiti, mafunzo na ushirikiano kati ya vyuo vikuu, sekta ya viwanda na jamii ili kupata suluhu za changamoto za maendeleo na kuchochea maendeleo endelevu katika nchi za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Dkt. Mwamba ametoa rai hiyo Ofisini kwake Treasury Square jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa AICAD ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Prof. James Njiru, kuhusu kuimarisha ushirikiano na shughuli za taasisi hiyo yenye makao makuu yake jijini Nairobi, Kenya.