Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

Taarifa kwa umma kuhusu mkopo wa Uviko 19

06 Nov, 2021 Download

DODOMA: Tarehe 8 Septemba, 2021: BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeridhia kutoa mkopo nafuu kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa jumla ya dola za Marekani milioni 567.25 sawa na shilingi trilioni 1.3 kwa ajili ya kukabliana na athari za UVIKO-19.

Fedha hizo zinajumuisha mkopo nafuu usio na riba kupitia dirisha la Rapid Credit Facility (RCF) wa jumla ya dola za Marekani milioni 189.08; na mkopo nafuu wenye riba ndogo kupitia dirisha la Rapid Financing Instrument (RFI) wa dola za Marekani milioni 378.17.

Fedha hizo zitatumika ndani ya mwaka huu wa fedha katika kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii zitokanazo na UVIKO-19. Sekta zitakazonufaika kulingana na makubaliano yetu na IMF ni afya, elimu, utalii, maji, pamoja na kusaidia kaya maskini kupitia mfuko wa hifadhi ya jamii (TASAF) na kuwezesha makundi maalum ya vijana, wanawake na wenye ulemavu.