WIZARA YA FEDHA YAZIASA TAASISI ZA SERIKALI KUFUATA SHERIA NA MIONGOZO YA UKOPAJI, MISAADA NA DHAMANA

Wizara ya Fedha imezitaka Taasisi za Serikali kuhakikisha kuwa zinafuata Sheria na Miongozo ya ukopaji fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na taasisi hizo. Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Madeni, Wizara ya Fedha, Bwana Omary Khama, wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili kwa Taasisi za Serikali kuhusu matakwa ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada namba 134 pamoja na miongozo mbalimbali katika kufadhili miradi ya maendeleo.