WIZARA YA FEDHA YAWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUPATA ELIMU YA MISAMAHA YA KODI NANENANE

Wananchi wamehimizwa kufika kwa wingi katika Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya Kilimo (Nanenane) Kitaifa yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Jijini Dodoma, ili kupata elimu kuhusu misamaha ya kodi inayotolewa na Serikali katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kama chachu ya kukuza sekta hizo nchini. Wito huo umetolewa na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uchambuzi wa Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Fronto Furaha, alipokuwa akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda hilo.