WIZARA YA FEDHA YATWAA TUZO UANDAAJI BORA HESABU KWA MWAKA WA FEDHA 2022
Wizara ya Fedha Fungu 50 Huduma za HAZINA imekuwa mshindi wa kwanza na kufanikiwa kupata tuzo ya waandaji bora wa hesabu kwa mwaka wa Fedha ulioishia 30 Juni 2022 katika kundi la Wizara na Idara za Serikali zinazojitegemea. Tuzo hiyo imetolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA), jijini Dar es salaam.