WIZARA YA FEDHA YATOA MAFUNZO MFUMO WA UANDAAJI NA USIMAMIZI WA BAJETI (CBMS)

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, amefungua Kikao kazi cha mafunzo ya Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa ambacho kitaambatana na kufanya tathmini ya utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2023/2024 ili kuweka mikakati itakayosaidia kuboresha uandaaji wa mipango na bajeti kwa mwaka 2025/2026. Akizungumza jijini Dodoma kwa niaba ya Katibu Mkuu Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kupata mafunzo ya Mfumo wa CBMS ulioboreshwa na kujadili kuhusu mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/2024 ili kubaini maeneo ya kuboresha.