WIZARA YA FEDHA YATOA MAFUNZO KWA WAZABUNI KUTOKA BOTSWANA

Wataalamu kutoka Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni ya Ununuzi wa Umma nchini Botswana wameipongeza Tanzania kwa kuwa na mifumo imara ya ununuzi na utatuaji wa migogoro ya ununuzi hatua inayochangia kupata wazabuni na wakandarasi wernye sifa za kutekeleza miradi ya maendeleo. Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Msajili wa Mamlaka ya Zabuni ya Ununuzi wa Umma nchini Botswana, Bw. Geoffrey Gotshega, akiongoza ujumbe walipofanya ziara ya mafunzo Wizara ya Fedha na Mipango kujifunza mambo mbalimbali kuhusu utekelezaji wa sera za ununuzi.