WIZARA YA FEDHA YATOA ELIMU YA KURIPOTI MASUALA YA BAJETI KWA WAMILIKI WA KITANDAO YA KIJAMII

Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya habari imeahidi kufanya kazi kwa pamoja hasa katika kipindi hiki cha Bajeti kuelekea uwasilishwaji wa Bajeti Kuu ya Serikali inayotarajiwa kuwasilishwa Bungeni hivi karibuni. Hayo yameelezwa na Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi Salome Kingdom, katika Kongamano la Elimu kwa Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii Nchini yaliyofanyika mjini Morogoro katika ukumbi wa mikutano wa NaneNane.