WIZARA YA FEDHA YASHAURIWA KUWAFIKIA WANANCHI WOTE

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, Bi. Grace Quintine, ameishauri Wizara ya Fedha kuhakikisha Watanzania wote nchini wanapatiwa elimu ya fedha ili waweze kuwa na uelewa mpana wa masuala ya fedha na waweze kufanya maamuzi sahihi katika matumizi sahihi ya vipato vyao. Bi. Quintine ametoa ushauri huo alipokutana na Timu ya Wataalamu ya Wizara ya Fedha ambayo ilifika wilayani Urambo mkoani Tabora, kutoa elimu ya fedha kwa Wananchi ili waweze kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika Sekta ya Fedha na kujikomboa kiuchumi.