WIZARA YA FEDHA YAKABIDHI KADI ZA BIMA YA AFYA KWA WANAFUNZI SHULE MAALUM BUIGIRI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, amekabidhi kadi 100 za Bima ya Afya za Mfuko wa Bima ya Taifa (NHIF) kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Maalum ya Wasioona, Buigiri, iliyoko Wilayani Chamwino mkoani Dodoma. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi kadi hizo iliyofanyika katika shule hiyo, Bi. Omolo alisema kadi hizo sehemu ya kutekeleza ahadi iliyotolewa na watumishi wanawake wa Wizara hiyo mwaka 2023.