WIZARA YA FEDHA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI.
Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau wa Sekta ya Fedha nchini, inaendelea na zoezi la utoaji elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali ikiwemo Wahamasishaji wa Biashara ya Huduma Ndogo za Fedha, Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo, Vikundi vya Kijamii vya Huduma Ndogo za Fedha, Watoa Huduma za Fedha, Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Mahitaji Maalum.
Lengo la kutoa elimu hiyo ni kuhakikisha inaongeza idadi kubwa ya watu wenye uelewa mpana wa masuala ya fedha na kupata maarifa juu ya upatikanaji na utumiaji wa huduma rasmi za kifedha.