WIZARA YA FEDHA YAANZA KUTEKELEZA MKAKATI WA KUTOA ELIMU YA FEDHA
Wizara ya Fedha imeanza kutekeleza mpango wake wa kutoa elimu ya fedha vijijini awamu ya kwanza kwa baadhi ya mikoa ikiwemo Mkoa wa Singida ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya kifedha ikiwemo kukabiliana na mikopo umiza, matumizi bora ya fedha na utunzaji wa fedha binafsi na kuweka akiba.
Hayo yameelezwa na Afisa Usimamizi wa Fedha, kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Kimaro, Wilayani Manyoni mkoani Singida wakati akitoa elimu ya fedha kwa wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo.