WIZARA YA FEDHA YAAGIZA TAASISI ZILIZOISABABISHIA SERIKALI HASARA YA BILL. 8.7 KUCHUKULIWA HATUA

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) ameziagiza Mamlaka zote zinazohusika na makosa ya jinai hususan Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuzichukulia hatua kali za kisheria Taasisi 12 za umma zilizoisababishia Serikali hasara ya shilingi bilioni 8.77. Alitoa agizo hilo jijini Dodoma baada ya kupokea Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).