WIZARA YA FEDHA KUENDELEA KUIMARISHA SEKTA YA FEDHA

Serikali kupitia Wizara ya Fedha, inaendelea kutekeleza mageuzi yanayolenga kuimarisha sekta ya fedha, kuboresha upatikanaji wa fedha, na kuendeleza jukumu la ushirikishaji wa sekta binafsi katika ukuaji wa uchumi. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), alipokutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Kikundi cha Benki ya ECOBANK, ulipomtembelea ofisini kwake Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma.