WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KITAIFA KUPUNGUZA KIWANGO CHA UMASIKINI

Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Sekta ya Fedha nchini wameandaa Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yatakayotoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutumia huduma rasmi za fedha ili kujikwamua kiuchumi na kupunguza kiwango cha umasikini nchini. Hayo yameelezwa jijini Arusha na Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja alipokutana na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo yatakayofanyika tarehe 20 hadi 26 Novemba, 2023 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini humo.