WAZIRI WA FEDHA NA RC DODOMA WAANGAZIA FURSA ZA KIUCHUMI DODOMA

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa Mkoa wa Dodoma una fursa nyingi za kiuchumi na kijamii katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, biashara, utalii na madini ambazo zikiendelezwa na kuchangamkiwa ipasavyo zitakuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi na watu wake. Mhe. Balozi Omar amesema hayo alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, ofisini kwake jijini Dodoma kwa ajili ya kujitambulisha, baada ya hivi karibuni kuteuliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa Waziri wa Fedha.