WAZIRI WA FEDHA NA MKURUGENZI WA BENKI YA DUNIA WAJADILI UTEKELEZAJI MIRADI

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na na Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia, anayeziwakilisha pia nchi za Malawi, Zambia na Zimbabwe, Bw. Nathan Belete, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo wamejadili kuhusu utekelezaji wa program mbalimbali zinazofadhiliwa na Benki hiyo hapa nchini. Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Balozi Omar, aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuwa mshirika muhimu wa maendeleo ya Tanzania na kwamba Serikali inathamini kwa kiwango cha juu uhusiano huo wa muda mrefu, ushirikiano ambao umechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi kupitia ufadhili wa miradi mbalimbali ya kimkakati ya kiuchumi na kijamii.