WAZIRI WA FEDHA AZIHIMIZA TAASISI ZA FEDHA KUPUNGUZA RIBA NA GHARAMA ZA MIKOPO
Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omar (MB), ametoa wito kwa Taasisi za Fedha nchini kupunguza riba na gharama nyingine za mikopo ili kuwawezesha wananchi wakiwemo vijana kupata mitaji ya kuwekeza kwenye shughuli zao za kiuchumi.
Mhe. Balozi Omar ametoa rai hiyo wakati akifungua Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB katika Mkutano Mkuu wa 31 wa Wanahisa hao, uliobeba kauli mbiu ya “Vijana na Uwekezaji kwenye Hisa” inayofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
