WAZIRI WA FEDHA AMEIAGIZA BODI YA MICHEZO YA KUBAHATISHA KUDHIBITI MICHEZO HARAMU
Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar ameitaka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini (Gaming Board of Tanzania) kuhakikisha inasimamia vema sekta hiyo ili kudhibiti madhara katika jamii hususan kwa vijana.
Rai hiyo ameitoa Ofisini kwake Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Bodi hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Balozi Mstaafu Modest Jonathan Mero, kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi.
Mhe. Balozi Omar alisema kuwa, michezo ya kubahatisha imeruhusiwa kisheria imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza pato la Taifa lakini ni muhimu ikaendelea kusimamiwa vizuri.
