WAZIRI WA FEDHA AKIWASILISHA MAKADIRIO NA MAPATO YA WIZARA YA FEDHA 2024/25

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuiidhinishia Wizara yake makadirio ya mapato na matumizi ya kiasi cha shilingi trilioni 44.19, kati ya makadirio ya shilingi trilioni 49.35 za Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2024/2025, ili iweze kutekeleza vipaumbele vyake vitano ilivyopanga kuvitekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2024/2025. Ameeleza kuwa kati ya kiasi hicho kinachoombwa, shilingi trilioni 29.42 zitakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Misaada na mikopo inatarajiwa kuwa shilingi trilioni 5.13, mikopo ya kibiashara kutoka nje na ndani ya nchi inakadiriwa kuwa shilingi trilioni 9.60 na maduhuli ni shilingi bilioni 45.01.