WAZIRI WA FEDHA AKABIDHI MAGARI MAPYA 72 KWA TRA KUIMARISHA HUDUMA NA UKUSANYAJI KODI
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), leo tarehe 25 Februari, 2026, amekabidhi magari mapya 72 kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma katika maeneo mbalimbali nchini ili kurahisisha kuwafikia walipakodi, kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuboresha huduma kwa wananchi.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika Chuo cha Kodi, jijini Dar es Salaam, Mhe. Balozi Omar alisema kuwa Serikali itaendelea kuiunga mkono TRA katika kukidhi mahitaji muhimu ya kiutendaji, ikiwemo magari hayo mapya yaliyogharimu shilingi bilioni 24.8.
