WAZIRI WA FEDHA AIAGIZA TUME YA PAMOJA YA FEDHA KUTOA USHIRIKIANO.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameiagiza Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC), kushirikiana na Serikali kuchambua na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kuboresha huduma kwa Watanzania kupitia mapato ya Serikali za Mitaa pamoja na uwezeshaji unaofanywa na Serikali Kuu kwenda Serikali za Mitaa. Mhe. Balozi ametoa agizo hilo jijini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Tume ya Pamoja ya Fedha, ukiongozwa na Katibu wa Tume hiyo, Bw. Ernest Mchanga, walipomtembelea ofisini kwake Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma, kwa ajili ya kujitambulisha.