WAZIRI MKUU MHE. MAJALIWA ATOA WITO VYA MADHEHEBU YA DINI KUHIMIZA HIFADHI YA MAZINGIRA

SERIKALI imetoa wito kwa viongozi wa dini nchini kuhamasisha utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayotishia mustakabari wa Taifa kutokana na madhara yanayojitokeza dhahiri ikiwemo ukame na upungufu wa mvua. Wito huo Umetolewa mjini Arusha na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, wakati wa Ibada maalumu ya kustaafu kwa Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Bw. Brighton Kilewa na kuingizwa kazini Katibu Mkuu mpya wa Kanisa hilo Mhandisi Robert Kitundu, ibada iliyofanyika katika Usharika wa Ngarenarok, Dayosisi ya Kaskazini Kati.