WAZIRI MKUU MAJALIWA AFANYA ZIARA OFISI YA SOKO LA HISA DAR ES SALAAM

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuwa Serikali imeweka Sera, Sheria na Taratibu zinazolenga kuchochea biashara, uwekezaji na ukuaji wa uchumi nchini. Hayo yamesemwa kwaniaba yake na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akizungumza wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, katika Ofisi za Soko la Hisa la Dar es Salaam, Morocco, Jijini Dar es Salaam.