WAZIRI MKUU AAGIZA WANANCHI WAHAMASISHWE KUTUMIA HUDUMA RASMI ZA FEDHA.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Fedha kuandaa mpango maalum wa kutoa elimu na hamasa kwa Watanzania ili kila mmoja ajenge tabia ya kutumia huduma rasmi za fedha. Alitoa agizo hilo jijini Arusha wakati akizindua Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini humo, yenye kaulimbiu ya “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi".